×

Naibu Waziri Wa Afya Dkt. Mollel Awajulia Hali Majeruhi Wa Ajali Arusha

Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel leo Februari, 25, 2024 amewajulia hali majeruhi 21 wa ajali iliyohusisha magari manne eneo la Ngaramtoni, Mkoani Arusha waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mount Meru.

Dkt. Mollel amesema majeruhi wote wanaendelea vizuri na mmoja ndo kapewa Rufaa ya kwenda hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC Mkoani Moshi.

“Rais Samia Suluhu Hassan ametuelekeza majeruhi wote wa ajali hii kupatiwa matibabu bila kulipa gharama zozote”,

Dkt. Mollel ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu wakati wakiendelea kuwatibia majeruhi na kwa wale waliopoteza ndugu zao utaratibu wakupatiwa miili unaandaliwa na wataalamu.

Leave a Comment