
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ambalo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.3 hadi kukamilika kwake,
Fedha hizo ambazo zinatolewa na Serikali kuu ni kwa ajili ya Ujenzi wa jengo la utawala, ujenzi wa uzio kuzunguka jengo na ununuzi wa samani za ofisi.

Akizungumza wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo, Mhandisi wa Halmashauri hiyo Maige Gibai amesema ujenzi wake utasaidia kusogeza karibu huduma karibu na wananchi ambapo awali walikuwa wanasafiri takribani kilomita 90 kwenda Musoma mjini.

Aidha, amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo.
📍Musoma-Mara
🗓️Februari 29, 2024