
Ligi Kuu England inaendelea tena leo Machi 3, 2024 huku mbio wa ubingwa zikiendelea kupamba moto wakati Mabingwa watetezi, Manchester City wakichuana na Manchester United kwenye ‘Derby’ ya Jiji la Manchester.
Man City ambao wapo nafasi ya pili wakiwa pointi nne nyuma ya kinara Liverpool wanahitaji ushindi huku wakiangazia kutwaa ubingwa wa EPL kwa msimu wa nne mfululizo.
City wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na rekodi bora ya kutopoteza kwenye mechi 18 za michuano yote (ushindi 16 , sare 2).
Mara ya mwisho United kuzuru katika dimba la Etihad, ilipokea kichapo cha 6-3 huku Erling Haaland akifunga hat-trick na kutoa ‘assist’ mbili.