
NYOTA wa zamani wa Real Madrid, Jesé Rodríguez Ruiz ‘Jese’, anaripotiwa kutumia euro 5000 (Sh mil 13.7) katika kutuma ujumbe mfupi wa maneno ‘SMS’ kwa lengo la kumng’oa mpenzi wake wa zamani, Aurah Ruiz kwenye shindano ya Big Brother Hispania.
Fowadi huyo Mhispania ambaye kwa sasa anakipiga timu ya Coritiba inadaiwa hakufurahishwa na kitendo cha mpenzi wake huyo kushiriki mashindano hayo mwaka 2018 hivyo akalazimika kutenga fungu hilo la pesa kwa ajili ya kutuma SMS za kumuondoa kwenya kinyang’anyiro hicho.