×

Rais Samia Ahudhuria hafla ya The Citizen Rising Woman, Asema Alitaka Kuwa Muhudumu Wa Ndege – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya The Citizen Rising Woman tarehe 08 Machi, 2024

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema wakati anasoma sekondari ndoto yake ilikuwa ni kuwa mhudumu wa ndege kwa kuwa alivutiwa na wafanyakazi Shirika la Ndege la DRC wanavyovaa.

Rais Samia ameyasema hayo Ijumaa, Machi 8, 2024 wakati wa mahojiano ya ana kwa ana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd (MCL), Bakari Machumu kwenye kongamano la The Citizen Rising Woman linalofanyika ukumbi wa The Super Dome jijini Dar es Salaam.

Rais Samia  akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited (MCL) Bakari Machumu wakati wa hafla ya The Citizen Rising Woman katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Machi, 2024.
Rais Samia akipiga makofi pamoja na viongozi wengine.
Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla The Citizen Rising Woman.
Rais Samia akitoa Tuzo za The Citizen Rising Woman kwa Taasisi zilizofanya vizuri kwenye kutengeneza mipango ya kuwainua Wanawake kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome Masaki wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Machi, 2024.

RAIS SAMIA – ”NILITAKA KUWA MUHUDUMU wa NDEGE – NILIKUWA NAPENDA VIKOFIA VYAO – KAKA AKANIKATAZA”

Leave a Comment