
Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imetangaza adhabu kwa wachezaji na timu mbalimbali za Ligi Kuu.
Wachezaji wa klabu ya Simba, Kibu Denis na Mzamiru Yassin wametozwa faini ya Sh. 1,000,000 kila mmoja kwa kosa la kuondoa taulo la mlinda mlango wa Coastal Union litilokuwa limewekwa pembeni ya lango wakati mchezo ukiendelea, jambo lililoashiria imani za kishirikina.
