×

Majaliwa Azitaka Halmashuri Kuweka Mpango Wa Ufuatiliaji Na Tathmini Ya Matumizi Ya Ardhi

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezielekeza Halmashauri zote zinazotekeleza mradi wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Vijiji kuandaa mpango wa ufuatiliaji na tathmini ili kupima ufanisi wa utekelezaji wa mradi huo.

Ametoa maelekezo hayo leo Ijumaa, Machi 22, 2024 wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Kujadili Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi uliofanyika wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Waziri Mkuu pia amezielekeza Halmashauri zote ziandae mpango mahsusi wa kupata suhulu ya migogoro inayohusu mipaka ya vijiji. “Lengo la Serikali ni kupima ardhi yote nchini ili wananchi wakiwepo wanavijiji waweze kuitumia katika kufanya shughuli za kiuchumi, Wenyeviti wa Halmshauri hakikisheni mnatoa ushirikiano kwa Timu inayotekeleza mradi ili mapungufu yaliyopo yapatiwe suluhu”.

“Nisisitize Wakuu wa Wilaya, Wakurugnzi wa Halmashauri, Wenyeviti na Watendaji katika vijiji washiriki kikamilifu kuwafikia wananchi na kuwaelimisha umuhimu wa matumizi sahihi ya ardhi, ili waweze kunufaika pamoja na kupata hati miliki za ardhi wanayoimiliki” ameeleza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu pia amewataka Watalaam wa sekta ya ardhi, kushirikiana na viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji katika hatua zote za utekelezaji wa mradi.

Amesema kuwaelimisha Viongozi hao kutawasaidia katika kuhamasisha wananchi, lakini pia kutoa elimu kuhusu masuala ya ardhi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda, amesema mradi huo unategemea kutekelezwa katika Halmashauri za Wilaya zilizoko kwenye mpaka wa kimataifa wa nchi, Wilaya zenye migogoro mingi ya matumizi ya ardhi na Wilaya zenye fursa kubwa za kiuchumi.

ACT WAZALENDO WATISHIA KUJITOA SERIKALI ya UMOJA wa KITAIFA ZANZIBAR – ADO SHAIBU AFUNGUKA..

Leave a Comment