×

Tigo Yachaguliwa Kuwania Tuzo Ya ITU WSIS 2024 Kupitia Mradi Wa UCSAF

Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo imechaguliwa kuwania Tuzo ya ITU WSIS 2024 kupitia mradi wa UCSAF (Mfuko wa mawasiliano kwa wote)-Zanzibar.
Mradi wa Tigo wa Mawasiliano ya vijijini huko Zanzibar kwa ushirikiano na UCSAF umependekezwa kuwania Tuzo za ITU WSIS 2024.
Mradi huo umechaguliwa baada ya kufanikiwa kushughulikia changamoto za mawasiliano kwa kutambua maeneo 42 katika kata 38 kwa kupitia Serikali.

Tigo Zantel, kama mtoa huduma mmoja wa pekee, walikamilisha mradi huo kwa muda wa takriban chini ya mwaka mmoja ambapo watu 211,601 wamenufaika na mradi huo.

Leave a Comment