
Katika kuunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wanawake wanatumia nishati safi ya kupikia ili kuweza kutunza mazingira.
Akizungumza mapema leo Aprili, 4 ,2024 Mwanzilishi wabTaasisi ya Reflection Foundation na Balozi wa heshima Toka Visiwa vya Shelisheli, Mary Vonne Pool amesema kuwa wameona kuja kugawa mitungi hiyo ya gesi kwa kina mama wanaoishi maeneo ya Kisele, Kinene na Mwalisembe,Mkuranga kata ya Mwasembe lengo ni kuwafanya wakina mama wapikie nishati safi.

“Sisi kushirikiana na Oryx Energies tumetoka mitungi hii ya gesi ili kuwarahisishia wakina mama katika shughuli zao za kila siku na kuacha kukata Kuni pamoja na kupunguza gharama za ununuzi wa Mkaa ili mazingira yetu yaendelee kuwa salama kwa sababu miti inapikatwa inasababisha jangwa na kukosa mvua na kusabisha kukosekana kwa chakula.
“Hivyo niwaomba wakina mama wote ambao leo mmepata fursa hii, kuweza kutumia hiyo gesi na si kuuza kwa kuwa itawarahisishia katika matumizi ya jikoni na pia inawarahishishia kutumia muda mfupi katika mapishi,amesema Mary.
Nae County HSSEQ manager and ESA Ambassodar, Janeth Mutashobya ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu kutoka Oryx Energy Mr Benort Arnaud Arman, amesema kuwa wamegawa mitungi 400 kwa wamama hao ili kuwarahisishia katika majukumu Yao ya kila siku.
“Tumegawa hii mitungi ya gesi hivyo tunawapa elimu ya kutosha juu ya matumizi yake, hivyo basi wakina mama hawa wanatakiwa watumie wasiende kuuza kwa sababu itawasaidia wao na ikiisha sehemu ya kujaza tumewapa maelekezo ambapo Kuna msambazaji mkuu hapa tumeshawaonyesha.