×

TASAC: Watu 17 wameokolewa tukio la kuzama kwa Meli Kigoma

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa taarifa kuwa Watu 17 wameokolewa katika tukio la kuzama kwa Meli ya MV Maman Benita iliyokuwa inatoka Kigoma kuelekea Kalemie Nchini DR Congo katika Ziwa Tanganyika ikiwa na Abiria 27, Aprili 6, 2024

Taarifa imeeleza kuwa baada ya kuzama Aprili 7, 2024, Wavuvi walimuokoa Abiria mmoja raia wa China na hadi Saa 1:00 Usiku wa Aprili 7, 2024, Watu 17 waliokolewa (Wachina 2, Watanzania 3 na Wakongo 12). Chanzo cha kuzama kwa meli hiyo bado hakijajulikana huku Nahodha akiwa ni kati ya waliookolewa

TASAC imeeleza meli hiyo iliyozama eneo la Kabimba, DRC iliyosajiliwa chini ya Bendera ya DRC ilikuwa na Raia wa Tanzania (5), China (4), DRC (16), Kenya (1) na mtoto mdogo

Leave a Comment