×

Kada wa Chadema Atimukia CCM Buchosa

MCHUNGAJI wa Kanisa la yesu Milango la uzima  na kada wa Chadema, Stephano Msabila amekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mchungaji huyo na kada wa Chadema aliyetimukia CCM aliwahi kuwa Mwenyekiti wa kitongiji cha Isaka stoo kwa  miaka mitano na mjumbe Halmashauri ya Kata ya nyehunge kupitia chama hicho.
Baada ya kurudisha kadi na kuhamia CCM amesema ameamua kuhamia CCM ili afanye kazi kwa ukaribu na Serikali iliyokomadarakani.
” Mimi ni mchungaji nilikuwa nakuosa amani waamini wangu walikuwa wanapungua kutokana na kuwa Chadema hivyo nimeamua kurudi CCM ili niwe huru ,amesema Msabila.
Mbunge wa Buchosa Mhe. Eric Shigongo amepongeza hatua ya mchungaji huyo kuachana na Chadema na kuhamia CCMna kwamba amefanya uamuzi sahihi hivyo CCM ni chama sahihi.
Amewaomba wana CCM kumpatia ushirikiano mchungaji huyo ili aweze kutekeleza majukumu yake.
Baadhi ya wanaCCM wamesema mchungaji Stephano Msabila na kada wa Chadema kuhamia CCM ni hatua ya kufuta upinzani ndani ya Buchosa kutokana na alivyokuwa mwiba kwenye siasa ndani ya Chadema.

Leave a Comment