×

Shigongo, Chatanda Washiriki Mazishi ya Aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT Sengerema

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Taifa, Mary Chatanda amemwaga machozi alipokuwa akiaga mwili wa Jane Msoga aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Sengerema.

Jane Msoga alifariki April 30, 2024mwaka huu wakati akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure alipokuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.


Amesema UWT imepoteza mtu muhimu na mchapa kazi aliyekuwa akiipenda kazi yake na kwamba atakumbukwa daima na kuwataka wanachama wa CCM kuendeleza mshikamano ndani ya chama hicho.
“Wakati namaliza uchaguzi wangu na kutangazwa mshindi alikuwa mtu wa kwanza kunipongeza na kuniambia ninakwenda kuchapa kazi sitakuangusha na alikuwa mtu wangu wa karibu nitamkumbuka sana,” alisema Chatanda.

Ameongeza kuwa marehemu Msoga amehudumu kwenye nafasi yake ya Uenyekiti wa UWT Wilaya ya Sengerema kwa kipindi cha miezi 20 hadi alipofikwa na mauti.

Mchungaji wa Kanisa la AITC Mlima mjini Sengerema aliyeongoza ibada ya mazishi, Amos Ndugwa amesema hakuna siku wala saa ya kuondoka dunia hivyo tunatakiwa kujindaa sasa kwa kutenda mema kisha kumrudia Mungu.

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amemzunguzia marehemu Msoga kuwa alikuwa kiongizi shupavu aliyependa kazi yake na kuunganisha wananchi na wanachama wote wa CCM.


“Marehemu atakukumbukwa kwa misimamo yake ya kutaka haki na umoja na mshikamano,” amesema Shigongo.

Leave a Comment