×

Miezi Mitatu Kazini Aongeza Mapato Kutoka Mil 59 Kwa Mwezi Hadi Mil 170

Halmashauri ya wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma imefanikiwa kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato kutoka wastani wa shilingi milioni hamsini na tano  kwa mwezi hadi shilingi  milioni miamoja sabini.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Kigoma Chiruku Chilumba amewaeleza waandishi wa habari mkoani humo kuwa ongezeko hilo limefikiwa katika  kipindi cha miezi mitatu toka  mwezi January hadi Aprili  mwaka huu .
Aidha Chilumba amewataka watumishi  kuendelea kufanya kazi kwa umoja na mshikamano ili kuongeza zaidi kiwango cha makusanyo akisisitiza kuwa fedha inapoongezeka inawezesha halmashauri kujiendesha vizuri katika kuwahudumia wananchi.
Kufuatia hatua hiyo baadhi ya watumishi wakiwemo wakuu wa Idara  wamempogeza mkurugenzi wa huyo kwa kuja mbinu shirikishi katika masuala ya ukusanyaji usimamizi na uibuaji wa vyanzo vipya vya mapato.
Katika bajeti ya mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya ya Kigoma ya mwaka 2022/23 wastani wa  makusanyo kwa mwezi ulikuwa shilingi milioni hamsini na tano kiwango ambacho kimeongezeka zaidi ya mara tatu katika bajeti ya mwaka 2023 /24.

Leave a Comment