Mama huyu amefika kueleza shida yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda kuwa mwanaye amelawitiwa na mpaka sasa anajisaidia damu.
Ameendelea kumueleza makonda kuwa hata alipojaribu kufika kwenye vyombo husika hakupewa ushirikiano na kuonekana msumbufu.
Umati wa watu katika mkutano huo wameishia kulia kwani jambo lililozungumzwa ni huzuni kubwa.