Muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili ambaye pia alikuwa msanii wa Bongo Muvi kupitia Kundi la Kaole Sanaa Group, Sara Mvungi amekanusha kuwa kuwa yeye siyo miongoni mwa waimba injili walioachana na waume zao baada ya kupata umaarufu.
Amesisitiza kwamba matatizo kati yake na mumewe yalianza kabla hajaanza kuimba injili na waliachana muda mrefu uliopita huku akidai kuwa kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.
“Niliachana na mume wangu baada ya kunipeleka polisi, tena kabla hata sijaingia kwenye mambo ya uimbaji sasa naumia mtu kunichafua mitandaoni kuwa umaarufu ulinifanya nishindwe ndoa yangu,” alisema Sara.