
Miongoni mwa mambo yaliyokuwa kivutio kikubwa nje ya Ukumbi wa Bunge asubuhi ya leo, ilikuwa ni uwepo wa roboti Eunice aliyekuwa akiwakaribisha wageni waliokuwa wakiingia bungeni kusikiliza makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Muda mfupi baadaye, picha na video za Roboti Eunice zimegeuka kuwa gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii.
Miongoni mwa wachangiaji, wanaonesh kufurahishwa na maendeleo ambayo Tanzania imepiga kwenye masuala ya teknolojia kiasi cha kumuunda Roboti Eunice mwenye uwezo wa kuongea na kupeana mikono na watu.