×

LHRC Yamuonya Oscar Oscar Kuacha kuweka maudhui ya Udhalilishaji dhidi ya Wanawake

Mwanahabari Oscar Oscar

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekemea Vitendo vya Udhalilishaji vinavyofanywa na Mwanahabari Oscar Oscar kupitia Habari Picha za Mzaha (Memes) anazozisambaza Mitandaoni

LHRC imenukuu Ibara ya 12 ya Katiba ya Tanzania inayolinda heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa Utu wa Mtu na inapinga ubaguzi, Mkataba wa kupinga aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake pamoja na Ibara ya 4 ya Mkataba wa Maputo

Aidha, taarifa ya LHRC imetoa Onyo kwa Mwanahabari huyo na kumtaka kuacha mara moja kuweka maudhui ya Udhalilishaji dhidi ya Wanawake ambayo yanafanya waonekane kama chombo cha starehe. Kinyume na hapo LHRC imesema itachukua hatua za Kisheria

VITA NZITO! MPINA na MAWAZIRI BUNGENI /AGIZO la RAIS SAMIA/VIFO vya UTATA/SERIKALI YAINGIA..

Leave a Comment