×

Waziri wa Kilimo Bashe Ajibu Sakata Aliloibua Mpina Bingeni – Video

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amejibu hoja ya mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina akisema amekosea kufanya uchambuzi wa utoaji wa mbolea za ruzuku kwa kuwa usajili wa wakulima unasajili wakulima wote lakini si kila mkulima ananufaika na ruzuku.

Bashe amesema hayo wakati akijibu hoja kwenye mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2024/25, jijini Dodoma leo Jumatano Mei 22, 2024.

Bashe amesema asilimia 25 ya wakulima wanaopata mbolea ambayo ameiona Mpina ni kwa wakulima wa mazao ya chakula pekee.

Leave a Comment