×

Video: Ngosha Akamatwa Tuhuma Za Kumuua Penina Kwa Kumkatakata Mapanga Bar

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kwa Kamanda Muliro leo Mei 24, 2024 limethibitisha kumkamata na kumshikilia Joseph Sanura ngosha (31) mkazi wa Goba Lastanza, Kinondoni kwa tuhuma mauaji ya mtu aliyejulikana kwa jina la Penina Rwegoshora (28) mkazi wa Goba center, Kinondoni.

Tukio hilo limetokea tarehe 23 Mei, 2024 majira ya 07:00 asubuhi huko maeneo ya Goba Center, Kinondoni eneo la Penina Pub.

Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi unaonesha kulikuwa na mgogoro wa kimahusiano kati ya mtuhumiwa na marehemu kabla ya kushambuliwa kwa panga na mtuhumiwa.

Upelelezi unakamilishwa ili mtuhumiwa afikishwe Mahakamani haraka iwezekanavyo.

Leave a Comment