Rais Samia asaini Kitabu cha Maombolezo ubalozi wa Iran nchini
Global Publishers May 25, 2024 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran nchini Tanzania kufuatia Kifo cha Rais wa Nchi hiyo Hayati Ebrahim Raisi kilichotokana na ajali ya Helikopta nchini Iran. Rais Samia alisaini Kitabu hicho katika Ubalozi wa Iran uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2024. Kushoto ni Balozi wa Iran hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Mei 24, 2024 amewasili katika Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini na kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo, hayati Ebrahim Raisi kilichotokana na ajali ya helikopta nchini Iran.
Hayati Raisi alifariki dunia Mei 19, 2024 mwaka huu kaskazini-magharibi mwa Iran, kwenye mteremko wa mlima katika eneo la Varzaghan, karibu na mpaka wa Azerbaijan Mashariki.
Wengine waliofariki katika ajali hiyo ni Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran, Hossein Amir-Abdollahian na maofisa wengine kadhaa.
Rais Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini Hossein Alvandi Bahineh mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo. …Rais Samia akiendelea kuzungumza na Balozi Hossein Alvandi Bahineh. Rais Samia akiwa kwenye picha na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini Hossein Alvandi Bahineh pamoja na Maafisa Mbalimbali wa Ubalozi huo .Rais Samia akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Ubalozi huo Oysterbay Jijini.
MAKONDA AMSIMAMISHA MKURUGENZI na KAMANDA POLISI WAELEZE JAMAA WALIOKUTWA na RISITI FEKI WAPO WAPI