
KLABU ya mazoezi ya Bondwa Hiking ya Mkoani Morogoro kwa kushirikiana na jeshi la polisi Mkoani humo limefanya matembezi ya Kms 15 na mbio za Hisani Kms 30 lengo likiwa ni kuunga mkono wito wa waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa la kuwata wananchi kushiriki mazoezi ya ili kuweza kupambana na magonjwa mbalimbali yasio ambukiza.
Mbio hizo ziliongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda Ya Morogoro Mhe. Latifa Mansoor kwa kushirikiana na maafisa askari wa jeshi la Polisi,watumishi wa Mahakama pamoja na baadhi ya joking club zilizopo mkoani humo
Aidha katika mbio hizo kuligawanyika kundi jingine ambalo lilotembea umbali wa KM 15 kuzunguka maeneo tofauti ya Ndani ya Manispaa ya Morogoro.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kanda ya Morogoro Mhe Latifa Mansoor Mwenye Nguo za Pink akiongoza Mbio zilizoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa Kushirikiana na Club ya Bondwa Hiking
