×

Rais Samia Awasili Jamhuri ya Korea kwa ajili ya Ziara ya Kikazi ya siku sita

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Jeshi wa Seoul, Jamhuri ya Korea kwa ajili ya Ziara Rasmi ya Kikazi tarehe 31 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Samia Suluhu Hassan leo Mei 30, 2024 amewasili Jamhuri ya Korea kwa ajili ya Ziara ya Kikazi ya siku sita.

Katika ziara hiyo ya Rais Samia, Serikali ya Tanzania itaingia mikataba saba ukiwamo wa msaada na mkopo nafuu wa Dola za Marekani 2.5 bilioni kutoka katika Serikali ya Korea Kusini.

Pia Rais Samia atahudhuria mkutano mkuu wa nchi za Afrika na Korea utakaofanyika Juni 3 na Juni 4.

Rais  Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Jeshi wa Seoul, Jamhuri ya Korea kwa ajili ya Ziara Rasmi ya Kikazi tarehe 31 Mei, 2024.
Rais Samia akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Jeshi wa Seoul.
Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya Watanzania wanaoishi Jamhuri ya Korea.
Rais Samia akimtazama mtoto mara baada ya kuwasili.
Rais Samia akifurahia jambo na Wanadispora.

Leave a Comment