×

Mwakinyo Akalisha Mghana Kwa ‘Tko’ Ashinda Ubingwa wa WBO, Dar – Video

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo usiku wa kuamkia Juni 02, 2024 ameshinda Ubingwa wa WBO kwa TKO kwa kumpiga Bondia Mghana Patrick Allotey kwenye Ukumbi wa Warehouse uliopo Masaki, Dar es Salaam aliyeshindwa kuendelea na pambano round ya pili akidai ameumia bega.

Pambano hilo lilipangwa kuchezwa  Juni 01, 2024 lilishindwa kufanyika kwasababu mwakilishi wa WBO Afrika, Samir Captain kutoka nchini Ghana kushindwa kufika ukumbini.

Mwakilishi huyo ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu alishindwa kutokea licha ya kupigiwa simu na badala yake aliamua kujifungia hotelini kwa muda wote.

Mwakinyo alisema sababu iliyokwamisha pambano “Kuna changamoto kidogo imejitokeza, inabidi pambano letu sisi lisimamiwe na rais wa WBO ambaye yupo Dar es salaam lakini kuna changamoto zilitokea katika utafutaji wa malipo yake kutokana na changamoto ya kupatikana kwa Dola, mzee ametafutwa na hapatikani kwenye simu, tumejiandaa vya kutosha na tuna utayari wa kupigana lakini kinachoweka uzito ni hicho, nina hamu ya kukata kiu ya Mashabiki

Leave a Comment