×

Waziri Aweso amtumbua Mkurugenzi Mtendaji wa ROMBOWSSA

TAARIFA KWA UMMA

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Hamidu Aweso (Mb) amemuondoa katika nafasi yake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ROMBO (ROMBOWSSA), Mhandisi Martin Kinabo kwa mujibu wa kifungu cha 17(1) cha Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Sura ya 272 kikisomwa kwa pamoja na kifungu cha 48(1)(a) cha Sheria ya Kutafsiri Sheria Sura 1.
Kutokana na hatua hiyo taratibu za ofisi za kujaza nafasi hiyo zinaendelea.

Akizungumza na Menejimenti ya Wizara ya Maji Mhe Aweso ameeleza sababu ya kufanya maamuzi haya kwamba ni kutoridhishwa na utendaji kazi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji ya Rombo na kutoridhishwa na mwenendo huduma ya Maji kwa wananchi sambamba na utekelezaji wa Miradi na ufanisi wa Mamlaka ya Maji kwa ujumla wake.

Waziri Aweso amesema hii ni hatua ya awali katika kuendelea kusinamia ipasavyo utendaji kazi na ufanisi wa Mamlaka za Maji nchini na kuahidi kuendelea kufanya tathimini ya Mamlaka zote katika muktadha wa kutoa huduma stahiki kwa wananchi, uendeshaji, kusimamia na kutekeleza miradi ya Maji.

Leave a Comment