×

Bei Za Mafuta Zapanda, Kuanza Kutumika Leo Juni 5, 2024… Dar Petrol ni Tsh. 3261, Dizeli Tsh. 3122

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kushuka kwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa Nchini zitakazotumika kuanzia leo Jumatano June 05, 2024 saa 6:01 usiku ambapo kwa mwezi huu wa June 2024, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ni Tsh. 3261 kwa lita, dizeli Tsh. 3122 na mafuta ya taa 3261.

EWURA imesema mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi June 2024 yamechangiwa na kupungua kwa bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia (FOB) kwa wastani wa asilimia 11.82 kwa mafuta ya petroli, asilimia 7.77 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 7.94 kwa mafuta ya taa, kuongezeka kwa wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni (Applicable Exchange Rate) kwa 1.4%”

 

Leave a Comment