MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian, ameishauri Hifadhi ya Taifa ya Saadani kuangalia uwezekano wa kuwasiliana na Shirika la teli TRC ili kuona namna ambavyo usafiri wa njia ya reli utaweza kutumika kwa ajili ya wageni wanaotaka kutembelea hifadhi hiyo.

Mkuu huyo wa Mkoa alitoa Ushauri huo alipotembelea Maonesho ya biashara na utalii 2024 (Tanga Trade Fair) yaliyokuwa yakifanyika viwanja vya shule ya Sekondari ya Usagara iliyopo Jijini Tanga
Katika maonesho hayo, Mkuu huyo wa Mkoa alipata fursa ya kutembelea banda la hifadhi ya Taifa TANAPA ambapo alielezwa mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwenye sekta ya utalii hapa nchin
Pamoja na kuelezwa mafanikio kadhaa, RC Balozi Batilda Burian ndipo alihoji mpango uliopo kwa hifadhi hiyo ya Taifa ya Saadani katika kutumia njia ya reli kusafirisha wageni watakaohitaji kutembelea vivuto vya utalii eneo hil
“Leo nilikuwa nikiongea na Wazee wakanambia kwanini tusizungumze na wenzetu wa TRC wakaweka kituo kwa ajili ya Safari za Train kufika hifadhi ya Taifa ya Saadani,upo uwezekano huo upo kweli?” alihoji Mkuu huyo wa Mkoa
Katika majibu ya TANAPA kwa Mkuu wa Mkoa, kutoka kwa kamishina msaidizi wa uhifadhi Tanapa Kanda ya Mashariki Fredrick Malisa amesema tayari mawasiliano yamefanyika na Uongozi wa Shirika la reli TRC na wamekubali kujenga kituo cha reli kwenye eneo husika na Saadani itakapokuwa tayari imetakiwa kuwasiliana na uongozi wa Shirika la reli

“Tulishaongea na wenzetu wa TRC wakatuambia tukiwa tayari tuseme na wameshakitengeneza kile kituo hivyo hilo jambo linawezekana na kwa mwaka huu tulianza na mkusafirisha wageni ambao walikuwa watu 300 kufika hifadhi ya Taifa ya Nyerere”alisema
Mbali na hayo Kamishina Malisa alisema,wameyatumia maonesho ya mwaka huu ya biashara na utalii kuhamasisha wageni kutembelea maeneo ya hifadhi za Taifa huku wakiwajulisha kuwa huko kuna futsa za uwekezaj
“Watu wanakaribishwa kufanya uwekezaji kujenga Hoteli, kambi za muda na zile za kudumu kwa ajili ya wageni au watalii kufikia” alisema

Katika Mkoa wa Tanga kuna hifadhi za Taifa za Saadani na Mkomazi na kwa mujibu wa afisa huyo wa TANAPA gharama za kutembelea maeneo hayo ni rafiki na kwamba Maonesho ya mwaka huu yamekwenda vizuri kwa vile wamepatikana watu wengi wameonesha nia kwenda kutembelea hifadhi hizo. mai.. . . o.i.. elea hifadhi hizo.