MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare, amesema mazishi ya aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Isihaka Sengo, yamesimamiwa na serikali na amezikwa na watu wasiozidi kumi.
Loata amesema hakukuwa na sababu ya kusubiri majibu ya kitabibu kutoka maabara ya Dar kwani tayari muongozo ulishatolewa kuwa hakuna mikusanyiko.
Mazishi yamefanyika leo, Aprili 28, 2020, katika makaburi ya Kibwe katika manispaa hiyo na waliohudhuria ni watu wachache wa serikali na wachache wa familia.
