×

Aida Aibuka Mshindi Wa Zigo La Euro Na Hisense Kutoka Tigo, Akabidhiwa Tiketi Yake

Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa, Bi. Mary Rutta (kushoto) akikabidhi mfano wa tiketi kwa mmoja wa washindi wa Safari ya kwenda Ujerumani promosheni ya Zigo la Euro na Hisense Wiki ya Tatu, kulia ni Afisa Masoko wa Kampuni ya HISENSE Bwn. Joseph Mavura na kulia kwa Mary Rutta ni Balozi wa Pari mAtch, Mwaisa.   
Aida akifuraia baada ya kukabidhiwa mfano wa tiketi kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Tigo jijini Dar leo.                                                                                                                                                                                                                                            Aida Juma ameibuka mshindi wa Promosheni ya Zigo la Euro na Hisense kutoka Tigo, na amekabidhiwa tiketi yake na ataelekea nchini Ujerumani kushuhudia michuano ya UEFA 2024.
Ushindi wa Aida Juma unatokana na kutumia Tigopesa Super App kufanya manunuzi mbalimbali, kufanya miamala ya kutuma na kupokea pesa, kucheza mchezo wa kubahatisha na Parimatch.   Kampeni bado inaendelea ambapo jinsi ya kushiriki na kuingia kwenye droo ni kutumia huduma mbalimbali za Tigo kama vile kutumia huduma za Tigo Pesa kufanya miamala, kununua bando, vocha za kukwangua, kulipia huduma mbalimbali sehemu za biashara malipo ya serikali kama vile faini na mengineyo.

Leave a Comment