
Zikizotufikia ni kwamba uongozi wa mnyama umeanza mapema mipango ya kukisuka kikosi haswa eneo la ushambuliaji ambapo wameanza kuifuatilia saini ya mshambuliaji wa ihefu Elvis Rupia.
Rupia kabla ya kutua bongo alikuwa mfungaji bora katika ligi ya Kenya huku msimu huu akiwa amefunga tayari mabao 6 kwenye ligi kuu msimu huu.
Rupia licha ya kuwa ni mshambuliaji wa kati lakini amekua na uwezo wa kutokea pembeni kama winga wa kushoto na kulia jambo ambalo limewavutia Simba.
Simba msimu huu wamekuwa na changamoto katika eneo la ushambuliaji baada ya kuondoka kwa Baleke na Phiri jambo ambalo uongozi unatafuta washambuliaji wapya mapema.
Stori na Marco Mzumbe, GPL