
Maneno Ally (51) alikuwa meneja wa hoteli moja iliyopo Posta jijini Dar es Salaam, akiwa na ndoto nyingi maishani mwake.
Hata hivyo, ndoto zote zilizimika ghafla baada ya kuanza kuumwa na kugundulika kuwa alikuwa na saratani ya kiuno pamoja na saratani ya tezi dume.
Akizungumza kwa tabu, Maneno anasema yeye ndiye aliyekuwa mhimili wa familia ya watoto watano lakini kutokana na tatizo hilo amelazimika kulala kitandani kwa mwaka mzima huku mkewe akimkimbia kutokana na tatizo hilo.
Kwa sasa anahitaji kiasi cha shilingi Laki sita (600,000) ili kukamilisha matibabu ya mizunguko miwili ya mionzi.
Kama umeguswa, mchangie chochote kupitia namba 0787120463.
Ukiwa na shida inayohitaji msaada wa Watanzania, piga simu namba 0714 207395.