
Mrembo ambaye amewahi kubeba mataji mbalimbali ya urembo ikiwemo Miss Sinza, Miss Kinondoni na mshiriki wa Miss Tanzania 2010, Amisuu Maliki @amisuu_maliki amewaangukia Watanzania na kuomba msaada wa kuokoa maisha ya mama yake mzazi ambaye anahitajika kufanyiwa upasuaji wa haraka wa kukatwa mguu kwa mara ya tatu kutokana na mguu huo kuoza.

Akizungumza kwa uchungu na Global TV, Amisuu amesema kuwa hakuna mtu wa kumtegemea maana yuko na mdogo wake na hawana ndugu hivyo anahitajika milioni 40 kwa ajili ya kwenda India ili mama yake afanyiwe upasuaji wa haraka na kunusuru maisha yake.
Kama umeguswa na unataka kumsaidia chochote tuma kwa namba 0742 444 411 (Amisu Maliki)
