
Wananchi wameendelea kunufaika na Kampeni ya Zigo la Euro na Hisense inayoendeshwa na Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo kwa kujishindia zawadi mbalimbali zinazotolewa kwa washindi hao.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi zao washindi hao, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema;

“Ni siku nyingine ya furaha kwetu Tigo, Pari Match na Hisense kwani leo tunaendelea tena kutoa zawadi kwa washindi wetu katika Kampeni ya Zigo la Euro na Hisense.
“Mpaka sasa hivi tumeshapata washindi zaidi ya 24 waliojishindia zawadi mbalimbali, kuna waliojishindia pesa taslimu milioni moja moja, waliojishindia vifaa vya umeme ikiwemo Tv ya kisasa na friji ya kisasa na kuna waliojishindia zawadi kubwa kabisa ya kwenda kuangalia mechi za Euro mwaka huu 2024 nchini Ujerumani,” alisema.

Meneja huyo amesema pamoja na washindi hao kampeni hiyo bado inaendelea na nafasi za kujishindia bado zipo nyingi na kuwataka wananchi kuendelea kutumia Tigo Pesa Super App kufanya malipo yao yote ya bili mengineyo, kuweka pesa na Pari Match kwa kutumia Tigo Pesa Super App, ili waweze kuwa washindi wa zawadi hizo.
Aliendelea kusema kwa kutumia Tigo Super App utaweza kujishindia friji ya kisasa, Tv ya kisasa, pesa taslim na pia unaweza kujishindia zawadi kubwa kabisa ya tiketi ya kwenda kuangalia michuano ya Euro mwaka huu 2024 nchini Ujerumani na kusisitiza kwamba muda bado upo.

Kwa upande wao washindi hao kila mmoja alielezea furaha yake kwa ushindi huo na kuwasihi watumiaji wengine wa simu kutumia mtandao wa Tigo na kutumia Tigo Pesa Super App ili nao wajaribu bahati yao.