×

Live: Hali Tete Kenya! Maandamano Yanaendelea Mitaani Kupinga Bajeti – Mabomu Yapigwa Na Polisi…


Maandamano mengine ya kupinga Muswada wa Fedha wa 2024 yanafanyika leo (Jumanne) na Alhamisi kote nchini Kenya kujibu kutoridhishwa kwa umma na mapendekezo yaliyomo kwenye muswada huo.

Waandalizi wa maandamano hayo, vijana ambao wanafahamika kama Gen Z wanatoa wito kwa zaidi ya watu milioni moja kujitokeza na kushiriki.

Maandamano hayo yaliyopewa jina la “Kenya Reject-Finance Bill 2024,” yamekuwa yakishika kasi na kuwavuta maelfu ya watu mitaani wiki jana kutoa upinzani wao.

Kulingana na michakato ya bunge, leo hii ni hatua ambapo wabunge hupitia Mswada kifungu kwa kifungu kinachopendekeza marekebisho katika kile kinachojulikana katika lugha ya bunge kama kamati ya bunge zima.

Muswada huo ulipita awamu ya pili wiki iliyopita baada ya wabunge 204 kuunga mkono huku 115 wakiupinga. Baada ya hapo muswada huo utasogea awamu ya tatu ambapo Bunge litaupigia kura ukiwa na marekebisho mapya.

Waandamanaji wanahoji kuwa mpango wa kukusanya kodi zinazopendekezwa za katika muswada huo zitazidisha hali ngumu ya kiuchumi kwa Wakenya wa kawaida.

Usalama umeimarishwa karibu na majengo muhimu ya serikali, hasusan jijini Nairobi.

Vitengo vya usalama vimewekwa katika hali ya tahadhari , huku maafisa zaidi wakitumiwa kuzuia umati mkubwa unaotarajiwa.

Shule kote nchini zimeagizwa kufungwa mapema kwa mapumziko ya katikati ya muhula ili kuwaepusha wanafunzi kutokana na matokeo ya vurugu.

Waziri wa Usalama wa Ndani Kindiki Kithure ameonya dhidi ya majaribio yoyote ya kuvamia ofisi na miundombinu ya serikali.

Leave a Comment