×

Naibu Rais Kenya Amtaka Mkurugenzi Mkuu wa NIS Ajiuzulu

Bosi wa NIS Noordin Haji

Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua amekashifu Idara ya Kitaifa ya Ujasusi ambayo anadai ilishindwa kumjulisha Rais William Ruto kwa wakati kuhusu maandamano makubwa yaliyofanyika Jumanne. Gachagua alidai bosi wa NIS Noordin Haji alishindwa kumfahamisha Rais kuhusu ukubwa wa maandamano hayo kwa wakati ili kuepusha mauaji, vifo na uharibifu.

“Na ninamuhurumia bosi wangu Rais William Ruto kwa sababu habari hizi hazikupata,” Gachagua alisema.

Gachagua amesema hayo Jumatano Juni 25, 2025 katika makazi yake huko Mombasa, mji wa Pwani mwa Kenya ambapo amesema kufuatia kufeli kwake katika kutekeleza majukumu yake Haji anapaswa kujiuzulu.

“Iwapo Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi ingemweleza Rais miezi miwili iliyopita kuhusu jinsi wananchi wanavyohisi kuhusu Mswada wa Fedha wa 2024, Wakenya wengi hawangekufa, mali haingeharibiwa, afisi hazingeharibiwa. Hakungekuwa na fujo, lakini walilala kazini.”

Gachagua alisema ilibidi kufanya maandamano ya nchi nzima ili rais ajue ukweli kuhusu jinsi watu wanavyohisi kuhusu kodi mpya iliyopendekezwa katika Mswada huo “lakini kuna shirika ambalo limelipwa na umma ili kumjulisha Rais na serikali kuhusu hisia za watu wa Kenya”.

Pia alidai kuwa maafisa wakuu wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi walimwambia faraghani kwamba hawakuwa na habari za awali kuhusu ukubwa wa maandamano yaliyoandaliwa zaidi na vijana wa kizazi cha Gen Z.

Alisema kutokana na hali hiyo, vyombo vya usalama vilivyowekwa kuzima maandamano hayo vilishtushwa na ukali wa maandamano hayo.

”WAFANYABIASHARA KUGOMA WAHOJIWE WABUNGE – KUHUSU RAIS MWINYI – RUTO KAKOSEA” – KAMBAYA..

Leave a Comment