×

Wafanyabiashara Kariakoo wakubali Yaishe

Wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam wamefungua maduka yao na kuachana na mgomo na hatimaye kuendelea na biashara zao kama awali.

Picha ikionesha wafanyabiashara wa Kariakoo wakiendelea na majukumu yao

(Picha msaada wa Mtandao)

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kukutana na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma jana Juni 26, 2024.

Awali, wafanyabiashara hao walifunga maduka yao kushinikiza kero zao kusikilizwa na kutatuliwa na serikali ikiwemo kodi wanazokumbana nazo TRA.

Picha ikionesha wafanyabiashara wa Kariakoo wakiendelea na majukumu yao

(Picha msaada wa Mtandao)

Leave a Comment