×

Biden, Trump Wakabiliana katika Mdahalo wa Uchaguzi wa Rais – Video

Biden na Trump walikabiliana katika mdahalo kwenye makao makuu ya CNN mjini Atlanta.

Rais wa Marekani Joe Biden na mpinzani wake Donald Trump wamekabiliana katika mdahalo wa kwanza wa uchaguzi wa rais unaopangwa Novemba mwaka huu. Kila mgombea alitafuta kumpiku mwenzake katika mbio za White House.
Biden mwenye umri wa miaka 81, na Trump mwenye umri wa miaka 78, hawakusalimiana kwa kupeana mikono wakati waliposimama jukwaani katika studio za makao makuu ya televisheni ya CNN mjini Atlanta.

Hakukuwa na watazamaji ukumbuni na vipaza sauti vilizimwa wakati kila mmoja akizungumza.


Biden alifungua mdahalo kwa kumlaumu Trump kwa Uchumi ambao ulikuwa unaporomoka kwa kasi wakati alipochukua usukani na janga ambalo lilishughulikiwa vibaya mno, watu wengi walikuwa wanakufa.

Trump alijibu kwa kuishambulia rekodi ya utawala wa Biden. “Hajafanya kazi nzuri. Amefanya kazi mbaya. Na mfumuko wa bei unaiuwa nchi yetu. Hali hiyo inatuuwa kabisa,” Alisema Trump.

Trump pia alitoa madai ya kuwa “bora” katika mambo kadhaa, bila kutoa ushahidi. Wakati huo huo, Biden hakuridhisha sana katika mdahalo huo, akitoa majibu na sauti isiyo laini na wakati mwingine akionekana kuyapoteza Mawazo yake.

Hakukuwa na watazamaji katika ukumbi wa madahalo wa CNN

Leave a Comment