
Uongozi wa Klabu ya Yanga umetoa taarifa kuwa umepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyewahi kuwa Mdhamini na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Yusuf Manji. Taarifa hiyo imesema kifo cha Manji kimetokea leo June 30, 2024 Nchini Marekani alipokuwa akipatiwa matibabu.
Rais wa Yanga, Eng Hersi Said amesema enzi za uhai wake, Yusuf Manji alikuwa Kiongozi mahiri aliyejituma na kujitoa kwa ajili ya kuijenga Klabu ya Yanga
“Hili ni pigo kubwa kwetu Young Africans Sports Club na Familia ya michezo kwa ujumla, tutamkumbuka Yusuf Manji kwa mapenzi yake makubwa aliyokuvwa nayo kwa Club yetu na namna alivyokuwa akijitoa kwa hali na mali katika kuiendeleza sekta ya michezo Tanzania” — Eng Hersi
“Ndugu Yusuf Manji alihudumu katika nafasi mbalimbali za kiuongozi ndani ya Klabu yetu kama Mdhamini na Mwenyekiti ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa Mwanachama wa Young Africans Sports Club, Uongozi wa Young Africans Sports Club, unatoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa, Marafiki na Wanamichezo wote Nchini kwa msiba mzito wa Mpendwa wetu, tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu mahala pema Peponi, Amina” — Eng Hersi.
