×

Ibadilisheni Dawasa Ifanye Kazi Kama Sekta Binafsi – Waziri Aweso


Waziri wa Maji, Mhe.Jumaa Aweso(Mb) amewataka watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kubadilisha utendaji wa kazi na kuakisi mtindo wa sekta binafsi.

Waziri Aweso ameyasema hayo wakati akihitimisha ziara yake ya siku tano Mkoani Dar es salaam wakati akiongea na Watumishi wa mikoa ya kihuduma DAWASA Magomeni na Kinondoni ambapo ameelekeza watumishi kujikita katika kutoa huduma bora kwa wananchi na kujituma kutimiza wajibu wao kama watumishi wa Serikali bila kusubiri maelekezo ya viongozi wa juu.

Pia Waziri Aweso amechukua nafasi hiyo kumtambulisha Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire kwa watumishi na Viongozi wa Serikali na Chama Tawala walifika katika ziara hiyo na kumpa maelekezo ya kuhakikisha anatatua changamoto za kihuduma na kusisitiza kusimamia uzalishaji na usambazaji wa Maji kwa wakazi wa Dar es salaam na Pwani.

Leave a Comment