×

Sakata La Sukari: Bodi Haikuchelewa Kutoa Vibali vya Kuagiza Sukari, Mkurugenzi Mkuu Afunguka – Video

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari, Profesa Kenneth Bengesi.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari, Profesa Kenneth Bengesi amesema madai yaliyotolewa kwamba bodi hiyo ilichelewesha kutoa vibali va kuagiza sukari kwa wazalishaji wa ndani, hayana ukweli wowote.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 5, 2024 jijini Dar es Salaam, Profesa Bengesi amesema bodi ilitoa vibali mapema lakini wazalishaji ndiyo waliochelewa kuchukua vibali hivyo.

Ameongeza kuwa mbali na kuchelewa, kati ya kampuni zote za wazalishaji wa sukari nchini kwa mwaka 2023, ni moja tu ndiyo iliyoagiza sukari na kusababisha uhaba wa bidhaa hiyo nchini.

Leave a Comment