×

Riba Ya Benki Kuu Yasalia Asilimia 6, Naibu Gavana wa Benki Kuu Afunguka

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Yamungu Kayandabila.

Riba ya Benki Kuu katika robo ya tatu ya mwaka huu itaendelea kuwa asilimia 6 kama ilivyokuwa katika robo ya pili ya mwaka huu; Kamati ya Sera ya Fedha ya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania imetangaza.
Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha kilichofanyika tarehe Julai 2024.

Kiasi hicho kimefikiwa ili kutimiza malengo ya kiuchumi katika kipindi hicho, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Yamungu Kayandabila amesema wakati akitangaza uamuzi huo Julai 4, 2024 jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Gavana wa Benki Kuu, Emmanuel Tutuba.

Amesema, tathmini ya Kamati kuhusu mwelekeo wa uchumi na vihatarishi mbalimbali inaonesha kwamba utekelezaji wa sera ya fedha kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2024 umefanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei na kubaki chini ya lengo la asilimia 5.

“Kamati inatarajia uchumi wa ndani kuendelea kukua kwa kasi, sanjari na upatikanaji wa chakula cha kutosha, na kupungua kwa kasi ya kushuka kwa thamani ya shilingi kufuatia ongezeko la mapato ya fedha za kigeni kutokana na shughuli za utalii, pamoja na mauzo ya dhahabu na mazao ya biashara na chakula,” amesema.

Kuhusu mwenendo wa uchumi wa Tanzania, Gavana Tutuba amesema, Kamati imeridhishwa na kuendelea kuimarika kwa shughuli za kiuchumi, kutokana na utekelezaji wa sera thabiti na maboresho mbalimbali yenye lengo la kukuza uchumi.

Ameongeza kuwa hali ya kuimarika kwa uchumi inatarajiwa kuendelea katika siku zijazo, kufuatia hali ya hewa nzuri kwa ajili ya shughuli za kilimo, upatikanaji wa uhakika wa umeme, uboreshaji wa miundombinu, hususani reli, barabara, na bandari pamoja na sera na programu za maboresho.

Riba ya Benki Kuu kwa robo ya nne ya mwaka 2024 itatangazwa mwezi Oktoba mwaka huu . Hii ni kulingana na kalenda ya mikutano ya Kamati ya Sera ya Fedha ya mwaka.

MTAALAM ANAYEWATUNZA SIMBA – ”ANAISHI MIAKA 15 – AKIUMWA ANAJITIBU MWENYEWE – TUNAWAKAMATA”…

Leave a Comment