×

Prince Mpumelelo Dube Aanza Balaa Huko Yanga

Prince Dube

INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, Prince Dube ameanza kujifua akiwa na klabu yake hiyo mpya.

Rekodi itabaki kwamba Julai 8 2024 Dube ambaye ni muuaji anayetabasamu alikuwa na uzi wa kijani na njano na kuanza mazoezi kwenye changamoto yake mpya.

Ipo wazi kwamba aliibuka hapo akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na timu ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu Yusuph Dabo.

Dube amesaini dili la miaka miwili alifunga jumla ya mabao 7 msimu wa 2023/24 alipokuwa ndani ya Azam FC kabla ya kuamua kuvunja mkataba wake.

Mabingwa watetezi wa ligi Yanga wameshaingia kambini tayari kwa maandalizi kuelekea msimu wa 2024/25.
AlI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa wachezaji waliopo ndani ya kikosi hicho ni bora wanawapa nguvu ya kufanya vizuri zaidi.


“Tulifanya kazi nzuri msimu uliopita na tulikuwa na kikosi bora hivyo msimu ujao tunaamini tutakuwa bora zaidi na wachezaji watakuwa ni imara zaidi.”

MTOTO wa FAIZA na SUGU KUMBE ANAONA MATUSI ANAYOPEWA MAMA’KE IG-MAJIBU YATAKUVUNJA MBAVU

Leave a Comment