Kampuni ya Amsons Group ya Tanzania iliyojikita kwenye sekta za nishati, ujenzi, chakula na usafirishaji imeinunua Kampuni ya Bamburi Cement ya nchini Kenya kwa dola za Kimarekani milioni 180 (Takribani bilioni 513 za Kitanzania).
Mkataba huo unatajwa kuwa moja ya mikataba mikubwa zaidi ya kununua kampuni nyingine katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Amsons Group, kupitia kampuni yake tanzu ya Kenya, Amsons Industries Limited, imependekeza ofa ya kununua kila hisa kwa shilingi 65 (Kshs), ununuzi ambao unalenga kuimarisha uwepo wa Amsons katika sekta ya saruji ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Amsons Group, Edha Nahdi, alisema mkataba uliopendekezwa utaongeza wigo nafasi ya kundi hilo katika sekta ya saruji Afrika Mashariki kama sehemu ya maendeleo ya uchumi wa kanda na malengo ya ushirikiano wa masoko.