×

Dkt. Tulia Na Rais Putin Wajadiliana Namna Bora Ya Kuimarisha Amani Duniani (Picha +Video)

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (Kulia) akipngea jambo na Rais wa Urusi, Vladimir Putin Jijini St. Petersburg nchini Urusi

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi, Vladimir Putin Jijini St. Petersburg nchini Urusi leo Julai 12, 2024 ambapo katika mazungumzo yao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha amani Duniani.

Kuhusiana na mgogoro unaoendelea baina ya Urusi na Ukraine, Dkt. Tulia amesema “Kabla ya kuzungumza naye tayari tulishazungumza na Maspika wa nchi zote hizo mbili na sisi kama Umoja wa Mabunge Duniani tumezungumza naye kama Kiongozi wa nchi katika sura ambayo tunaweza kuziweka pamoja nchi zote mbili na tutarajie kwamba IPU itatengeneza fursa ya Mabunge ya pande zote ili kuweza kuzungumzia amani katika maeneo yao ya utawala”.

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Baraza la Shirikisho la Urusi, Mhe. Valentina Matvienko katika Ofisi ndogo za Baraza hilo zilizopo Jijini St. Petersburg nchini Urusi leo tarehe 11 Julai, 2024.
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, alipowasili St. Petersburg nchini Urusi ambapo alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Fredrick Kibuta Julai 10, 2024

Leave a Comment