
WATU maarufu duniani wamewasili Mumbai kwa ajili ya harusi ya mtoto wa kiume wa tajiri zaidi barani Asia, Mukesh Ambani.
Anant Ambani anatarajiwa kufunga pingu za maisha leo Julai 12, 2024 na Radhika Merchant, binti wa mfanyabiashara wa maduka ya dawa wa India Viren na Shaila Merchant, katika sherehe ya kitamaduni ya Kihindu kwenye jiji la Mumbai siku ya Ijumaa.
Sherehe za ndoa hiyo zitafanyika Julai 14, 2024

Hafla za harusi zilianza na sherehe mnamo mwezi Machi.
Sherehe hizo zilizochukua miezi kadhaa zimehudhuriwa na mastaa wakubwa wa Bollywood, wanamuziki na vigogo wa biashara kama vile Bill Gates na Mark Zuckerberg.

Siku ya Ijumaa, nyota wa televisheni Kim Kardashian, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair na rapa wa Nigeria Rema walikuwa miongoni mwa waliotua katika mji mkuu wa India kuhudhuria sherehe hizo.

Sherehe za harusi ya wanandoa hao huenda zikaendelea kwa siku kadhaa. Hafla zimepangwa kufanyika siku ya Jumamosi na Jumapili na sherehe kubwa ya mapokezi itafanyika siku ya Jumatatu.
Wasanii watao fanya shoo kwenye harusi hiyo ni Adele, Drake, Lana Del Rey, Sonu Nigam, Hariharan, Shreya Ghoshal Shankar Mahadevan, Shah Rukh Khan, Gauri Khan, Alia Bhatt, Ranbir Kapoor
