
Rais wa Marekani Joe Biden amekataa wito wa baadhi ya viongozi wa chama chake cha siasa kuachia azma yake ya kugombea kufuatia mdahalo na Donald Trump mwezi uliopita ambapo Biden mara nyingine alipata shida kujieleza.
Kama Biden siyo mteuliwa wa chama cha Democratic, nani atakuwa mteuliwa? Mwandishi wa VOA Scott Stearns anawaangazia baadhi ya wagombea.
Rais Joe Biden anasema yeye yuko katika kinyang’anyiro ili kushinda.
Rais Joe Biden anasema: “Nadhani mimi ni mtu mwenye sifa za kugombea urais.”
Kufuatia kufanya vibaya katika mdahalo mwishoni mwa mwezi uliopita, baadhi ya viongozi wa chama chake wanamtaka Biden kuachia ngazi kama mgombea mtarajiwa.
Lakini baada ya upigaji wa awali na majimbo, chama cha Democratic hakiwezi kumlazimisha kuondoka, anasema Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Virginia kituo cha siasa Larry Sabato.
Larry Sabato, Chuo Kikuu cha Virginia alieleza: “Kuna njia moja tu kwa mteule kuondolewa, na hiyo ni kwa mteule kuamua kutowania kabla ya mkutano mkuu, kufungua, kuruhusu katika kesi hii, Kamati ya Kitaifa cha Democratic, kuweka kanuni kwa ajili ya mkutano mkuu.”
Kama Biden ataamua kuondoka, makamu rais na mgombea mwenza Kamala Harris atakuwa juu katika orodha ya Democratic kuchukua nafasi yake.
Harris anasema Biden ni mteule wa chama na ameonyesha utiifu wake kwa kumdharau Trump, ambaye ametengana na makamu rais wake wa zamani Mike Pence.
Kamala Harris, Makamu Rais wa Marekani amesema: “Fahamu kati ya Joe Biden na Donald Trump, ni mgombea mmoja tu katika hilo jukwaa ameidhinishwa na makamu wake wa rais – Joe Biden.”
Harris kama mteule wa chama huenda akasaidia kwa upande wa wapiga kura huru, anasema profesa wa sayansi ya siasa wa Chuo Kikuu cha Southern California, Christian Grose.