×

Ona Mapokezi ya Rais Samia Mkoani Katavi Atakagua na Kufungua Miradi – Picha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wananchi wa Mpanda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mpanda mkoani Katavi tarehe 12 Julai, 2024. Rais  Dkt. Samia ameanza Ziara ya Kikazi Mkoani humo ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi
Rais Samia akipokea taarifa ya maboresho ya kiwanja cha ndege cha Mpanda pamoja na jengo la abiria kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura, mara baada ya kuwasili uwanjani hapo Mkoani Katavi tarehe 12 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yupo mkoani Katavi amewasili katika mkoa huo Julai 12, 2024.

Rais Dkt. Samia ameanza Ziara ya Kikazi Mkoani humo ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi

Leave a Comment