
Malkia wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga almaarufu Nandy ameamua kutoa ya moyoni kuhusu mahaba anayopewa na mumewe ambaye pia ni msanii mwenzake, William Lyimo au Billnass baada ya ndoa yao kutimiza miaka miwili tangu ifungwe.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Official Nandy amesema ndoa yeke imekuwa fundisho kubwa kwenye maisha yake na kumfanya ajue nini maana ya upendo.
“Mume wangu miaka miwili ya ndoa yetu imekuwa fundisho kubwa kwangu kujua upendo ni kitu muhimu sana, uwepo wako umerahisisha maisha yangu na ya kipenzi chako NAYA jua tu tunakupenda sana. Nachokuomba najua wanaume mmeumbiwa kupepesa macho japo siyo mwanaume wangu wewe (joke) popote uendapo, chochote ufanyacho jua una watu wanakupenda na kukuhitaji sana, kuyashinda majaribu now days ni rahisi sababu kila kitu kishapitwa na wakati na wakati wenyewe ndo sasa kuonyesha mfano na kuwa mifano bora kwa watu wenye mapenzi ya kweli kuwa vijana wakiamua inawezekana. MUNGU wangu atulinde nitimize ahadi ya watoto wako 10 NAKUPENDA PY @billnass HAPPY ANNIVERSARY MY LOVE” ameandika Nandy The African Princess.