
Wananchi Kenya wako huru kukusanyika na kufanya maandamano baada ya Mahakama Kuu nchini humo kupinga uamuzi wa Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi, Douglas Kanja wa kupiga marufuku maandamano ya umma yaliyopangwa na vijana jijini Nairobi.
Jaji wa Mahakama ya Juu Bahati Mwamuye amesema hakuna afisa wa polisi anayeruhusiwa kutekeleza agizo lililotolewa na Kanja mnamo Julai 17, akisubiri kusikizwa kwa ombi lililowasilishwa na Taasisi ya Katiba.
Kanja alipiga marufuku maandamano kwa muda usiojulikana akisema maandamano yamesababisha sio tu uharibifu mkubwa wa mali bali pia watu wengi kupoteza maisha kutokana na wahalifu kujipenyeza.