×

Rais Samia Azungumza Na Machifu Chamwino Ikulu, Akemea Matukio ya Utekaji (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  akizungumza na Machifu kutoka Mikoa mbalimbali nchini, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye viwanja vya Ikulu kwa ajili ya kuzungumza na Machifu kutoka Mikoa mbalimbali nchini, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Anazungumza na Machifu Chamwino Ikulu Dodoma leo tarehe 20 Julai, 2024.

Rais Samia ameonesha kukasirishwa na ‘drama’ za matukio ya utekaji anayoendelea kutokea nchini na kuwaagiza viongozi wa ngazi ya jamii wakiwemo kukemea matukio hayo.

Amesema kwa miaka yote Tanzania imekuwa ikisifika kama nchi ya amani ambapo matukio hayo yanapotokea, yanachafua taswira ya nchi huku akieleza kuwa mengi huwa ni ya kutengenezwa na jamii yenyewe na mwisho lawama kutupwa kwa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Akiwa kwenye picha ya pamoja na Machifu kutoka Mikoa mbalimbali nchini katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Julai, 2024.

Leave a Comment