Kampuni ya Sukari Kilombero ilipewa heshima kubwa ya kuikaribisha tena timu ya ‘Illovo Sugar Africa Kilimanjaro Climber’, baada ya kurejea salama kutoka kwenye kilele cha mlima huku wakisindikizwa na chapa maarufu ya “Bwana Sukari.”
Tukio la kuwakaribisha tena limefanyika katika lango la Marangu na kulakiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Utalii, sambamba na timu ya Bodi ya Utalii Tanzania.
Katika hafla hiyo ya kufurahisha kikundi hicho kilikabidhiwa vyeti vya ushindi wao wa kupanda Mlima Kilimanjaro na kufikia kilele cha Uhuru katika mwinuko wa mita 5895/19841 kutoka usawa wa bahari.
Tukio hili la aina yake linasimama kama msingi wa Kampeni ya ‘Kilimanjaro Expedition’.
Maazimio ya pamoja ya kuupanda mlima Kilimanjaro yalikuwa kwa ajili ya kuheshimu urithi usiofutika wa Mandela na kuchangisha fedha na uhamasishaji katika mapambano dhidi ya hedhi salama, katika kuhakikisha wasichana 20,000 wanasaidiwa kupitia nchi ambazo Illovo Sugar inatoa huduma kwa kutoa taulo za kike kwa mwaka mzima.
Sherehe ya kuwakaribisha wageni hao ilifana sana na uwepo wa Naibu Katibu Mkuu wa Utalii Ndugu Nkoba Mabula akishirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania sambamba na mwakilishi kutoka Kampuni ya Sukari Kilombero ambapo Kampuni hiyo ya Sukari ni mwenyeji wa wageni hapa nchini.
Katika hafla hii muhimu, Naibu Katibu Mkuu wa Utalii Bw. Nkoba Mabula aliwapongeza wapanda mlima wote kwa kurejea salama wakiwa na furaha na mshikamano. Alisisitiza nia thabiti ya Serikali katika kusaidia na kuwezesha sekta ya utalii, kuhakikisha mazingira yanasaidia shughuli za Utalii.
Akiwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, Bw. Mabula aliwapongeza wapanda mlima huo kwa kufanya ziara ya kupanda kilele cha mlima Kilimanjaro, wakitumia jitihada hizo kukusanya fedha za kukabiliana na hedhi salama kwa watanzania na jamii nyinginezo ambako Kampuni hizo zinafanya kazi, ikiwa na dira ya ustawi wa jamii ni kuwa na maendeleo.
Akizungumza katika hafla ya kuwakaribisha wageni hao, Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Sukari Kilombero, Ndugu: Derick Stanley, alisisitiza jukumu kubwa la nchi mwenyeji katika kuhakikisha jitihada za kutangaza kivutio cha mlima Kilimanjaro zinafanikiwa.
Alisisitiza umuhimu wa kuonyesha utofauti na ushirikishwaji kwa ushiriki wa vikundi mbalimbali vya wapanda mlima, hivyo kudhihirisha fahari ya Tanzania kama nchi mwenyeji na Mlima Kilimanjaro kuwa kivutio cha watalii.
Ndugu, Derick aliipongeza zaidi hatua ya chapa ya ‘Bwana Sukari,’ kufikishwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro na wawakilishi wa Tanzania, kuashiria ubora wa bidhaa hiyo, uwepo wake sokoni, na utofauti katika mlima huo mkubwa. Kampuni ya Sukari Kilombero inawatakia kheri wapanda mlima wote amani na furahi wanapoendelea kufurahi vivutio vya nchini Tanzania.
Kwa upande mwingine, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), mshirika mkuu katika Kampeni hii ya ‘Kilimanjaro Expeditions’, ikiwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Ephraim Balozi Mafuru imeliona tukio hili kama kichocheo cha kukuza vivutio vya utalii nchini na imejikita kusaidia mipango ya kuendelezea sekta ya utalii.
Kama ishara ya kushukuru wakati wa hafla ya kuwakaribisha wageni hao, timu iliyoongoza wapandaji ikiongozwa na, Dk. Ernest Peresu, ilionyesha shukrani ya dhati kwa ukarimu wa watanzania na maliasili nyingi za Tanzania, na kuwahimiza watu duniani kote kuja na kushiriki katika kufurahia vivutio vya aina yake vinavyopatikana Tanzania.
Kampuni ya Kilombero ambayo ni kampuni tanzu ya ‘Illovo Sugar’, itabaki imara katika kuhakikisha inakuza ustawi wa jamii kupitia Kampeni mbalimbali kama vile ‘Kilimanjaro Expeditions’, yenye lengo la kupambana na tatizo la hedhi salama.
Sambamba na ahadi hiyo, kampuni imetoa msaada wa taulo za kike 2400 kwa Shule ya Sekondari Mieresini iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro.